Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Ruvu (maana)
Chanzo | Milima ya Uluguru, mitelemko ya mashariki |
Mdomo | Bahari Hindi, karibu na Bagamoyo |
Nchi | Tanzania |
Urefu | km 285 |
Tawimito upande wa kulia | Mto Mgeta |
Tawimito upande wa kushoto | Mto Ngerengere |
Eneo la beseni | km² 17,700 |
Ruvu (zamani Kingani pia[1]) ni mto wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani nchini Tanzania.
Unapokea hasa maji ya upande wa mashariki wa milima ya Uluguru na kuyapeleka Bahari Hindi.
Ruvu hii haina uhusiano na mto Jipe Ruvu wa mkoa wa Kilimanjaro / Upare.