Sabino wa Canosa (Canosa di Puglia, Italia, 461 - Canosa di Puglia, 9 Februari, 566) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 514[1].
Rafiki wa Benedikto wa Nursia, alitumwa na Papa Agapeto I kwenda Konstantinopoli kutetea imani sahihi kuhusu utu halisi wa Yesu.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Februari[2].