Safari (kutoka Kar. سفر safar) ni neno la kutaja mwendo au harakati ya watu kutoka mahali fulani kwenda mahali pa mbali angalau kiasi. Safari inaweza kufanywa ama kwa miguu au kwa chombo cha safari au usafiri fulani. Kama safari inazidi muda wa siku mmoja vituo vya safari yaani mahali ambapo msafiri anakaa au analala hadi kuendelea ni sehemu za safari yake. Kuna safari ndefu na safari fupi. Harakati inayotumia muda mfupi tu kama dakika chache au kwa umbali mdogo huitwi safari isipokuwa kwa lugha ya kutaania.