Kuhusu kundinyota la Pisces linaloitwa pia "Samaki" angalia hapa
Samaki | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kundi la tengesi mkia-njano (Sphyraena flavicauda)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Kladi 5 za samaki:
|
Samaki ni wanyama wenye damu baridi wanaoishi kwenye maji ya mito, mabwawa, maziwa au bahari.
Wote ni vertebrata, yaani huwa na uti wa mgongo.
Wanatumia oksijeni iliyomo ndani ya maji kwa kuyavuta kwenye mashavu yao.
Kuna aina nyingi za samaki wadogo wenye urefu wa sentimita moja na wakubwa wenye urefu hadi mita 15. Ila tu viumbehai wakubwa kwenye maji si samaki bali nyangumi ambao ni mamalia.