Sao Hill

Sao Hill ni kata ya mji wa Mafinga katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51402.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 3,799 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,765 waishio humo.[2]

Sao Hill ina umbali wa kilomita 15 kutoka Mafinga mjini kando ya barabara ya TANZAM kuelekea kusini (Mbeya).

Kitovu cha Sao hill ni kiwanda cha kusaga mbao maana Sao Hill iko katikati ya misitu mikubwa ya kupandwa hasa ya miti ya misonobari na mikalatusi. Misitu hiyo ilianzishwa zamani za ukoloni na siku hizi zinashughulukiwa na kampuni ya Kinorwei ya Green Resources.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Iringa Region-Mafinga Town Council

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne