Saskatchewan







Saskatchewan

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Kanada Kanada
Mji mkuu Regina
Eneo
 - Jumla 651,900 km²
Tovuti:  http://www.sk.ca/
Hospitali ya Royal University ipatikanayo ndani ya jimbo la Saskatchewan

Saskatchewan ni jimbo la Kanada. Limepakana na Northwest Territories, Nunavut, Manitoba, Montana, North Dakota na Alberta.

Lina eneo la km² 651,900.

Kunako mwaka wa 2009, idadi ya wakazi ilikuwa 1,023,810.

Mji mkuu ni Regina na mji mkubwa ni Saskatoon.

Saskatchewan ni hasa jimbo la kilimo cha ngano pamoja na mafuta ya petroli.

Lugha rasmi ni Kiingereza.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne