Satelaiti

Sputnik 1 ilikuwa satelaiti ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu
Muonekano mzima wa Satelaiti ya kuchunguzia Dunia(Earth observation satellite ERS 2

Satelaiti (pia setelaiti, setilaiti, kutoka Kilatini satelles, "msindikizaji", kupitia Kiingereza satellite) ni kitu kinachofuatana na kitu kingine. Neno linatumiwa kwa maana mbili ambayo ni:

  1. magimba asilia katika anga-nje kama mwezi, na
  2. vifaa au vyombo vilivyotengenezwa na kurushwa na binadamu ili kuzunguka dunia kwa kazi mbalimbali, au kwa lugha nyingine vyombo vya angani. Satelaiti havibebi watu.

Kwa kufuata maana hii ya 2, Satelaiti au Setilaiti ni kifaa cha kuundwa na binadamu ambacho huundwa kwa kusudi la kukiweka kwenye obiti kwaajili ya shughuli maalumu kama vile utafiti wa kisayansi. Mara nyingine vifaa hivi huitwa satelaiti za kutengenezwa ili kuzitofautisha na satelaiti asilia kama vile mwezi wa Dunia.

Satelaiti ndogo aina za Cubesat zina umbo la mchemraba na uzito wa kilogramu moja tu; GhanaSat-1 iliyotumwa na wanafunzi wa Ghana mwaka 2017 ni Cubesat

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne