"Say Somethin'" ni wimbo ulioandikwa na Mariah Carey akishirikiana na Snoop Dogg, Chad Hugo, wakishirikiana na Pharrell Williams kwa ajili ya albamu ya Carey ya kumi iliyoitwa The Emancipation of Mimi iliyotoka mwaka 2005. Mwimbaji Snoop Dogg anatokezea katika wimbo huu kama mwanamuziki wa kushirikishwa na anaimba shairi moja. Wimbo huu unajumuisha waimbaji mbalimbali na ulifanikiwa kutoka rasmi mwaka 2006, kama single ya sita kutoka katika albamu hii. Wimbo huu ulifanikiwa kufika katika nyimbo arobaini bora nchini Australia na Uingereza, lakini nchini Marekani wimbo huu haukufanikiwa kuingia hata katika chati ya Billbord Hot 100.