Sekta ya anime imeendelezwa kwa kiasi kikubwa katika miaka michache iliyopita, hasa nje ya Ujapani. Imeenea kwa kasi duniani kote, pamoja na ongezeko kubwa katika kupatiwa kwa leseni zinazopatia kibali cha kuonyesha vipindi na filamu kwa maeneo mengi, vituo vya anime kama Animax pia vimeendelezwa. Animax kinakubaliwa kuwa kituo kikuu miongoni mwa vingine kinachotangaza vipindi siku nzima katika ulimwengu, [1] kinatangaza vipindi vya anime katika Ujapani, Taiwan, Hong Kong, Filipino, Bara Hindi, Marekani ya Kusini na Korea ya Kusini.