Serafino wa Montegranaro (1540 – 12 Oktoba 1604), alikuwa bradha wa shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini kutoka Italia ya Kati.
Fukara kweli, aling'aa kwa unyenyekevu na moyo wa ibada[1].
Mtawa huyo asiye na vipawa vingi kiutu, bali mwenye karama za ajabu, anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Klementi XIII tarehe 16 Julai 1767.