Setei

Kanisa kuu la Pescara, lenye jina lake.

Setei (karne ya 6 - 597 hivi) anatajwa kama askofu wa Amiterno (leo San Vittorino, katika mkoa wa Abruzzo, Italia) au wa Aternum (leo Pescara)[1] ambaye Walombardi walipovamia maeneo yale aliuawa kwa kutoswa mtoni amefungiwa jiwe kubwa shingoni kwa kusingiziwa kwamba alisaliti mji wake [2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Juni.[3]

  1. [1]
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/90550
  3. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne