Severo wa Barcelona

Sanamu yake katika kanisa kuu la Barcelona, kazi ya Bartolomé Ordóñez, mwaka 1519.

Severo wa Barcelona (alifariki Barcelona, Hispania, 304 hivi) alikuwa askofu ambaye inasemekana aliuawa kwa ajili ya imani ya Kikristo[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Novemba[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/76330
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne