Shady Records

Shady Records
Shady Records logo.png
Shina la studio Universal Music Group
Imeanzishwa 1999; miaka 26 iliyopita (1999)
Mwanzilishi
Usambazaji wa studio
Aina za muziki Hip hop
Nchi Marekani
Mahala

Shady Records ni studio ya kurekodi muziki kutoka nchini Marekani. Studio ilianzishwa na Eminem na meneja wake Paul Rosenberg mwaka 1999 baada ya mafanikio makubwa ya albamu ya Eminem The Slim Shady LP.[1]

Mwaka wa 2006, Shady ilitoa albamu iliyokwenda kwa jina la Eminem Presents: The Re-Up. Albamu hii ilishirikisha wasanii ambao walikuwa miongoni mwa washirika wa mwanzo wa lebo hiyo. Shady Records pia iliandaa nyimbo zilizotumika kwenye filamu iliyoigizwa na Eminem, 8 Mile. Wimbo wa "Lose Yourself" ulitumika kwenye filamu hii na ni wimbo wa kwanza wa hip hop kupokea Tuzo ya Akademi kwenye kipengele cha wimbo bora.

Washirika wa sasa wa Shady records ni pamoja na Eminem, Bad Meets Evil, Westside Boogie na Grip, wakati washirika wa zamani ni pamoja na D12, Obie Trice, 50 Cent, Stat Quo, Bobby Creekwater, Cashis, Slaughterhouse, Yelawolf, Griselda, Westside Gunn na Conway the Machine.

  1. "Loading..." www.hitquarters.com. Iliwekwa mnamo 2022-08-05.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne