Sherehe

Sherehe ya divai huko Soweto, Afrika Kusini (2009).

Sherehe (kutoka neno la Kiarabu) ni sikukuu muhimu inayoendana na shangwe.

Sherehe nyingi zina asili katika dini mbalimbali na zimeathiri sana utamaduni husika. Kati ya sherehe za namna hiyo kuna Diwali ya Mabanyani, Hanukkah ya Wayahudi, Krismasi ya Wakristo na Eid al-Adha ya Waislamu.

Sherehe nyingine zinaadhimisha mwendo wa mwaka, hasa majira, mazao ya kilimo, au matukio ya historia ya jamii husika, kwa mfano ushindi muhimu vitani, n.k.

Sherehe nyingi zinaadhimishwa mara moja tu kwa mwaka, linavyodokeza neno la Kilatini "sollemnitas" (kwa Kiingereza "solemnity").


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne