Shirika la Kenya la Wanyama Pori (KWS - Kenya Wildlife Service) lilianzishwa mwaka 1990. Inasimamia uasilia na viumbe hai wa nchi, ikilinda na kuhifadhi flora na fauna.
KWS inasimamia mbuga za wanyama za kitaifa na hifadhi nchini Kenya. Fedha zinazokusanywa kama ada ya kiingilio hutumika kusaidia uhifadhi wa mimea na wanyama ndani ya hifadhi au mbuga.