Shirikisho

Shirikisho ni muundo wa serikali ambako madaraka na mamlaka hugawanywa kati ya ngazi ya kitaifa na ngazi ya maeneo yanayojitawala katika mambo mbalimbali.

Mifano ya shirikisho ni:

  • Afrika Kusini ni maungano ya majimbo 9
  • Marekani ilianzishwa kama maungano ya koloni 13 asilia zilizoasi dhidi ya Uingereza mwaka 1776 na kukabidhi sehemu za mamlaka zao kwa serikali ya shirikisho
  • Nigeria ni Shirikisho la Jamhuri la majimbo 36
  • Urusi ni shirikisho linalojumuisha maeneo malimbali yenye ngazi tofauti za mamlaka ndani yake

Falsafa ya kisiasa katika shirikisho ni ya kwamba mamlaka inakabidhiwa kutoka chini kwenda juu. Hivyo serikali kuu imepewa mamlaka yake kutoka majimbo yake na haina madaraka ya kuondoa haki za majimbo.

Kinyume chake ni itikadi inayoweka mamlaka yote katika ngazi ya serikali kuu inayoweza kuamua kukabidhi sehemu ya madaraka yake kwa maeneo na vitengo vya kiutawala.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne