Sint Maarten (yaani Mtakatifu Martino) ni nchi ya visiwani katika bahari ya Karibi (Amerika ya Kati). Iko kwenye sehemu ya kusini ya kisiwa cha Saint Martin kilichogawiwa baina ya Ufaransa na Uholanzi.
Sint Maarten ilikuwa koloni la Uholanzi; sasa ni "nchi ya kujitawala" ndani ya muundo wa "Ufalme wa Nchi za Chini" pamoja na Uholanzi yenyewe na nchi nyingine zilizokuwa makoloni ya Uholanzi.
Katika eneo la kilometa mraba 37 wanaishi watu 40,120.
Lugha ya wengi (asilimia 67) ni Kiingereza, ikifuatwa na Kihispania.
Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti (karibu asilimia 50) halafu Wakatoliki (asilimia 33).