Sista Blandina (jina la kuzaliwa: Rosa Maria Segale; Cicagna, Genova, Italia, 23 Januari 1850 – Cincinnati, Marekani, 23 Februari 1941),[1] alikuwa mtawa wa Shirika la Masista wa Upendo la Cincinnati na mmisionari, ambaye alipata umaarufu kutokana na utumishi wake kwenye mipaka mipya ya Marekani mwishoni mwa karne ya 19.[2]
Wakati wa kazi yake ya kimisionari, alikutana na watu maarufu kama Billy the Kid na viongozi wa makabila ya asili ya Marekani, ikiwa ni pamoja na Waapache na Wakomanche. Alifanya kazi kama mwalimu na mfanyakazi wa kijamii katika maeneo ya Ohio, Colorado, na New Mexico, akiwasaidia Waindio, walowezi wa Kihispania, na wahamiaji kutoka Ulaya.[3]
Imeanzishwa kesi ya kumtangaza mtakatifu[4].
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)