Soukous | |
---|---|
Asili ya mtindo | Muziki wa dansi wa Kikongo, son cubano |
Asili ya utamaduni | Mwishoni mwa miaka ya 1930 nchini Kongo (hasa Kinshasa na Brazzaville) |
Ala | Gitaa (hasa la kufinyanga kidole), besi, ngoma, brasia, sauti |
Michanganyiko ya aina | |
Benga, Mbalax, Makossa, zouk | |
Inapotendeka | |
Midundo ya Kikongo (Kenya, Uganda, Tanzania), soukous ya mwendo-kasi (Paris) | |
Mada nyingine | |
Wanamuziki wa Soukous |
Soukous (pia inajulikana kama Lingala au rumba la Kikongo) ni jina la kutaja aina maarufu ya muziki wa dansi ambao umetoka katika Kongo katika miaka ya 1940, hasa ulitokana na athira ya Cuban son. Mtindo huu ulianza kupata umaarufu zaidi katika miaka ya 1960 na 70. Soukous hufahamika kama Lingala nchini Tanzania, Kenya, na Uganda hasa kwa sababu mashairi yake huimbwa kwa lugha ya Kilingala. Huko nchini Zambia na Zimbabwe, ambapo muziki wa Kikongo napo upo maarufu, bado huitwa kwa jina la rumba. Leo hii, unashikisha mitindo mingine kama vile kwasa kwasa na muziki wa kasi juu wa zouk.