Spaghetti Westerns (pia: Western za Kiitalia) ni aina ya filamu za Western zilizotolewa na studio za Italia kuanzia miaka ya 1960. Awali lilikuwa jina la utani tu kutokana na chakula cha Kiitalia cha spaghetti lakini mtindo ulipendwa baadaye na watu wengi.
Filamu halisi za huko zilikuwa zinarekodiwa kwa lugha ya Kiitalia na zilikuwa zitumia bajeti ndogo tu. Mara nyingi zilicheza na ujumbe wa mawestern ya Marekani na kubadilisha tabia za vielezo vya western kama vile cowboy, sheriff, jambazi na wengineo. Pia zilionyesha wazi matendo ya kishenzi, ujeuri n.k. yaliyofichwa zaidi katika western za Marekani.
Ni hasa mwongozaji Sergio Leone aliyeanzisha aina hiyo ya Western.