Stockholm

Kitovu cha kale cha Stockholm
Ramani ya Stockholm

Stockholm (pia Stokolimi) ni mji mkuu wa Uswidi na pia mji mkubwa wa nchi hito wenye wakazi 864,324 (31 Desemba 2011) ambao pamoja na rundiko la mji ni watu milioni 1.3.

Mji uko kwenye pwani ya mashariki ya Uswidi ambako ziwa Mälaren lajiunga na Bahari Baltiki. Kitovu cha mji ni visiwa 14 vinavyotengwa na mifereji yenye madaraja.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne