Sully Prudhomme (16 Machi 1839 – 7 Septemba 1907) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Ufaransa. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa René-François-Armand Prudhomme. Mashairi yake yanaonyesha sifa za ujumi. Mwaka wa 1901 alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Nobel kwa Fasihi.