Sydney Bristow | |
---|---|
muhusika wa Alias | |
![]() | |
Mwonekano wa kwanza | "Truth Be Told" (sehemu ya 1.01) |
Mwonekano wa mwisho | "All the Time in the World" (sehemu 5.17) |
Imechezwa na | Jennifer Garner |
Maelezo | |
Majina mengine | Bluebird Freelancer Mountaineer Phoenix |
Jinsia | Kike |
Kazi yake | Kachero ugani wa SD-6 CIA The Covenant muuaji (DSR kachero mara mbilit) APO kachero ugani |
Taji | Agent Sydney Bristow |
Ndoa | Michael Vaughn (mume) |
Significant other(s) | Danny Hecht (fiancé; deceased) |
Watoto | Isabelle Vaughn (binti, amezaa na Michael) Jack Vaughn (mtoto wa kiume, amezaa na Michael) |
Ndugu | Jack Bristow (baba; amefariki) Irina Derevko (mama; amefariki) Elena Derevko (mama mdogo; amefariki) Katya Derevko (mama mdogo) Nadia Santos (dada wa kufikia; amefariki) |
Utaifa | Mmarekani |
Sydney Anne Bristow (amezaliwa tar. 17 Aprili 1975) ni jina la kutaja muhusika mkuu katika mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Alias. Uhusika umechezwa na Jennifer Garner. Yeye ni mwanamke wa Kimarekani mwenye asili ya Kirusi-Kimarekani ambaye anafanya kazi kama mpelelezi wa CIA.
Sydney anaonekana katika mfululizo akiwa mama mshupavu kimuonekano na hata kihisia halkadhalika. Amekuwa akijishughulisha na baadhi ya kazi za viwewe vya maana kwa miaka zaidi: kifo cha mchumba wake, kifo cha rafiki yake wa karibu, kugundua kwake kwamba mama yake alikuwa mpelelezi wa zamani wa KGB, utenganisho wake na marafiki zake waliowengi na uwastani wa kazi yake na mabadiliko ambayo hana budi kuyavumilia kuwa mpelelezi na kuishi katika hali ya kawaida. Sydney ana maarifa ya hali ya juu katika Krav Maga na ni hodari sana wa malugha, anazungumza Kiingereza, Kirusi, Kijerumani, Kigiriki, Kiholanzi, Kifaransa, Kiitalia, Kihispania, Kireno, Kinorwei, Kiswidi, Kiromania, Kihungaria, Kiyahudi, Kiubzbeki, Kiarabu, Kiajemi, Kiurdu, Kiindonesia, Kikantonese, Kimandarini, Kijapani, Kikorea, Kihindi, Kivietnamu, Kipolandi, Kiserbia, Kicheki, Kiukraini, na Kibulgaria katika vipengele mbalimbali vya mfululizo. Katika mfulizo majina msimbo anayotumia ni pamoja na Bluebird, Freelancer, Mountaineer, na Phoenix.