Taarifa (kutoka neno la Kiarabu) ni habari maalumu inayowasilishwa ama kwa mdomo ama kwa maandishi.
Pia ni takwimu zilizochakatwa ambazo zina maana kamili inayoweza kutumika katika kufanya maamuzi fulani.
Mfano:
Taarifa hutofautiana kulingana na muktadha kama ilivyo kwa takwimu.
Taarifa ya habari ni wasilisho la maelezo ya tukio au hali maalumu kwa jamii nzima linalopitia njia yoyote: redio, gazeti, runinga, mbiu au mikutano.