Tangi ni chombo kikubwa kinachotumiwa kuhifadhia au kuwekea vimiminika au gesi[1]. Hutengenezwa kwa bati gumu, chuma, plastiki au dutu nyingine isiyoathirika na vitu vinavyohifadhiwa mle.
Tangi zinapatikana kwa maumbo tofauti na kila ukubwa. Tangi ndogo mfano ya kibatari hushika mafuta kidogo kama nusu thumuni ya lita, tangi la gari huwa na lita 50-60 na matangi makubwa yanayopatikana bandarini hushika lita milioni kadhaa yakipokea mafuta kutoka meli zinazobeba mafuta[2].