Tarakilishi, ngamizi au kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kukusanya taarifa (data), na halafu kuzishughulikia kulingana na kanuni za programu ya tarakilishi inayopewa. Inafuata hatua za mantiki katika kazi hii. Hapo hutoa matokeo ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana (information) kwa haraka.