Teresa Couderc (jina la kuzaliwa: Maria Viktoria; Mas de Sablieres, Ufaransa, 1 Februari 1805 – Fourvieres, Ufaransa, 26 Septemba 1885) alikuwa bikira wa Kanisa Katoliki ambaye, kwa moyo mtulivu kati ya tabu nyingi, alianzisha shirika la Masista wa Bibi Yetu wa Mafungo kwenye kijiji cha La Louvesh, karibu na kaburi la Yohane Fransisko Regis.
Aliongoza shirika hadi alipoondolewa madarakani na watu waliompinga (1838). Hapo alishika utiifu kikamilifu[1].
Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 4 Novemba 1951 halafu Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 10 Mei 1970.