Quintus Septimius Florens Tertullianus (160 hivi – 225 hivi),[1] alikuwa padri na mwandishi maarufu wa Ukristo wa mwanzoni kutoka Karthago, mji wa mkoa wa Afrika katika Dola la Roma, leo nchini Tunisia.[2]
Ndiye Mkristo wa kwanza aliyeandika sana kwa Kilatini, akiathiri fasihi yote iliyofuata hasa kwa misamiati yake mipya, hasa kuhusu fumbo la Utatu Mtakatifu[3] akaitwa "mwanzilishi wa teolojia ya Magharibi."[4]
Katika maandishi yake anajitokeza kama mtetezi wa imani pamoja na kupinga uzushi, ingawa ukali wa itikadi yake hatimaye ulimfanya ajitenge na Kanisa Katoliki[5].
Habari chache tulizonazo kuhusu maisha yake yanapatikana hasa katika maandishi yake.