Tha Trademarc |
---|
Marc Predka (anajulikana kwa jina la kisanii kama Tha Trademarc; alizaliwa 21 Aprili 1975) ni mwanamuziki wa Rap kutoka Marekani.
Mara ya kwanza kujulikana kwa umaarufu ilikuwa wakati yeye na binamu yake wa kwanza mwanamiereka wa WWE John Cena walishirikiana mnamo 2005 kutoa albamu You Can't See Me. Pia anaonekana katika video za nyimbo , ‘’Bad Bad Man’’ na ‘’Right Now’’ ambazo amefanya na John Cena. Leo hii yeye hufanya kazi katika kitengo cha elimu ya waiosjiweza katika Shule ya Maynard kule Maynard, Massachusetts.
Mnamo Agosti 2007, Trademarc alionekana katika miereka ya Total Nonstop Action Wrestling, ‘’Hard Justice’’ kama ‘’Mpenzi mpya’’ wa Karen Angle, ambayo baadaye ilithibitishwa kuwa uvumi wakati Karen na Trademarc walimsaidia bwanake Kurt Angle kushinda mechi[1].
Alionekana tena katika iMPACT! wiki iliyofuatia .[2]. Akiendelea kufanya kazi na TNA, alitoa wimbo wa kiingilio wa Kurt Angle ‘’Gold Medal’’ ambao aliufanya kwa kuchanganya rap kutoka Lunatic Fringe na utunzi wa TNA wa "My Quest". Mnamo 2008 alitoa solo Albamu yake ya kwanza Inferiority Complex.