The Notorious B.I.G.

The Notorious B.I.G.
Jina la kuzaliwa Christopher George Latore Wallace
Amezaliwa (1972-05-21)Mei 21, 1972
New York City, New York, United States
Amekufa 9 Machi 1997 (umri 24)
Los Angeles, California, United States
Aina ya muziki Hip hop[
Kazi yake Rapa, mtunzi wa nyimbo, mwimbaji, mtayarishaji wa rekodi
Miaka ya kazi 1992–1997
Studio Bad Boy
Ame/Wameshirikiana na Sean Combs, Method Man, Junior M.A.F.I.A., Total, 112, The Commission
Tovuti www.badboyonline.com/notoriousbig

Christopher George Latore Wallace (anajulikana kama Biggie Smalls, jina la jambazi la kwenye filamu ya mwaka wa 1975 ya Let's Do It Again, "The Black Frank White", jina la mwuza madawa ya kulevya katika filamu ya mwaka wa 1990 King of New York),[1] na hasa kwa jina la kisanii The Notorious B.I.G.; 21 Mei 19729 Machi 1997) alikuwa rapa kutoka nchini Marekani.

Alikulia Brooklyn, mji wa New York City, Wallace amekua kwenye kipindi cha matatizo ya uigaji tabia chafu kwenye miaka ya 1980, hivyo basi akaanza kujishughulisha na uuzaji haramu wa dawa za kulevya akiwa bado bwana mdogo kabisa. Wakati Wallace ametoa albamu yake ya kwanza yenye jina la rekodi ya mwaka 1994 Ready to Die, alikuwa umbo la kati kwenye uwanja wa East Coast hip hop na kuongeza mwonekano wa New York kwa kipindi hicho wakati wasanii wa West Coast tayari wamekuwa maarufu kwenye nyanja kuu za hip hop kitambo. Mwaka uliofuatia, Wallace akaongoza marafiki zake wa utotoni hadi kwenye mafanikio ya kichati kupitia kundi la wafuasi wake la Junior M.A.F.I.A.. Wakati anarekodi albamu yake ya pili, Wallace alijishughulisha sana na masuala ya kigomvi ya East Coast-West Coast, ilitawala katika uwanja wa hip hop kwa kipindi hicho.

Mnamo tar. 9 Machi 1997, Wallace aliuawa na watu wasiojulikana wakati anaendesha gari huko mjini Los Angeles. Seti yake ya diski mbili ya Life After Death, ilitolewa baada ya siku kumi na tatu baadaye, imegonga nafasi ya kwanza #1 kwenye chati za albamu nchini Marekani na kutunukiwa Almasi mnamo mwaka wa 2000.[2] Wallace alitambulika sana kwa staili yake ya "kujiachia, anachana taratibu", uwezo wa kimashairi yanayoeleza tawasifu kimtindo. Tangu kifo chake, albamu mbili zaidi zilitolewa. MTV wamweka nafasi ya #3 kwenye orodha yao ya Ma-MC Wakali wa Muda Wote.[3]

  1. Reid, Shaheem; Bland, Bridget. Kash, Tim Notorious B.I.G.: In His Own Words, And Those of His Friends Ilihifadhiwa 11 Machi 2007 kwenye Wayback Machine. MTV News, 2007-03-07. Retrieved on 2007-03-11
  2. "Top 100 Albums". RIAA. 4 Mei 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-22. Iliwekwa mnamo 2006-12-07.
  3. The Greatest MCs of All Time Ilihifadhiwa 18 Machi 2015 kwenye Wayback Machine. MTV. Retrieved on 2006-12-26

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne