Christian Matthias Theodor Mommsen (30 Novemba 1817 – 1 Novemba 1903) alikuwa mwanahistoria na mwandishi kutoka nchi ya Ujerumani. Anafahamika hasa kwa kitabu chake Historia ya Roma (kwa Kijerumani: Römische Geschichte). Mwaka wa 1902 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.