Theotoni (Ganfei, Ureno, 1082 hivi - Coimbra, 18 Februari 1162) alikuwa padri kanoni na mshauri wa mfalme wa Ureno Afonso I.
Alikwenda mara mbili kufanya hija Yerusalemu alipokataa uongozi wa Kanisa katika Nchi Takatifu.
Aliporudi kwao alianzisha monasteri ya Waaugustino huko Coimbra iliyostawi haraka [1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu; heshima hiyo ilithibitishwa na Papa Benedikto XIV.