Thomas Tafirenyika Mapfumo ni mwanamuziki wa Zimbabwe. Alizaliwa mnamo mwaka 1945[1] huko Marondera, Zimbabwe. Anajulikana pia kama "Simba wa Zimbabwe" kutokana na mchango wake kisiasa nchini Zimbabwe. Nyimbo zake zilipinga ubaguzi wa rangi kabla ya uhuru na siasa za serikali ya Robert Mugabe baadaye. Alipaswa kuondoka Zimbabwe akiishi Marekani sasa. Anapiga muziki aina ya chimurenga.