Thomas Menamparampil

Thomas Menamparampil S.D.B. (alizaliwa 22 Oktoba 1936 huko Pala, Kerala, India) ni Askofu Mkuu mstaafu wa Guwahati.

Alihudumu kama askofu wa Dibrugarh kwa miaka 11 na Askofu Mkuu wa Guwahati kwa miaka 20 hadi alipostaafu tarehe 18 Januari 2012. Aidha, alihudumu kama msimamizi wa kitume wa Dayosisi ya Jowai, nafasi aliyoteuliwa na Papa Fransisko kuanzia tarehe 3 Februari 2014 hadi 15 Oktoba 2016.[1]

  1. Menamparampil, Thomas (2003). Cultures in the Context of Sharing the Gospel (kwa Kiingereza). St Pauls. ISBN 9788171095766.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne