| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Honra, Pátria e Povo" (Kireno) "Heshima, Taifa na Watu" | |||||
Wimbo wa taifa: Pátria | |||||
![]() | |||||
Mji mkuu | Dili | ||||
Mji mkubwa nchini | Dili | ||||
Lugha rasmi | Kitetum, Kireno1 | ||||
Serikali | Jamhuri José Ramos-Horta Taur Matan Ruak | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilikubaliwa |
{{{established_dates}}} | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
15,007 km² (ya 159) kidogo sana | ||||
Idadi ya watu - Julai 2021 kadirio - Msongamano wa watu |
1,340,513 (ya 153) 78/km² (ya 137) | ||||
Fedha | U.S. Dollar3 (USD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+9) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .tl3 | ||||
Kodi ya simu | +670
- | ||||
1 Kiingereza na Kiindonesia vimekubaliwa na katika ya nchi kama "lugha za kazi". 2 Indonesia ilivamia Timor tar. 7 Desemba 1975 na kuondoka 1999. 3 Kuna pia sarafu za centavo ya Timors ya Mashariki. |
Timor ya Mashariki (kwa Kireno Timor-Leste, kwa Kitetum Timór Lorosa'e; jina rasmiː República Democrática de Timor-Leste au Repúblika Demokrátika Timór-Leste) ni nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki, takriban km 640 kaskazini kwa Darwin, Australia.
Eneo lake ni nusu ya mashariki ya kisiwa cha Timor pamoja na visiwa vya Atauro na Jaco. Kuna pia eneo dogo upande wa magharibi wa Timor ambao kwa kiasi kikubwa uko chini ya Indonesia pamoja na visiwa vya jirani.
Eneo lote la nchi ni km² 15,007.
Mji mkuu ni Dili wenye wakazi 245,000.
Timor ya Mashariki ni kati ya nchi maskini zaidi duniani.