Tour de France ni shindano mashuhuri la baisikeli nchini Ufaransa[1]. Lilianzishwa mnamo mwaka 1903 na kuendelea kufanyika kila mwaka katika mwezi wa Julai.
Jina Tour de France linamaanisha Ziara ya Ufaransa kwa sababu washiriki wanapitia Ufaransa yote katika muda wa wiki 3, na wakati mwingine sehemu za mbio zinaingia pia katika nchi jirani.
Linatazamwa kama shindano la mbio za baisikeli gumu zaidi duniani.[2] Washiriki ni wanaume pekee.