Trudo (pia: Tron, Trond, Trudon, Trutjen, Truyen; Hesbaye, leo nchini Ubelgiji, 628 hivi - Hesbaye 693 hivi) alikuwa mmonaki padri aliyeanzisha monasteri mbili huko kwao alipokusanya wanafunzi wengi baada ya kutoa mali yake yote kwa Kanisa la Metz [1][2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Novemba chake[3].