Tutankhamun (pia: Tutankhaten, Tutankhamen) alikuwa farao wa Misri ya Kale. [1] Alitawala tangu alipokuwa na umri wa miaka tisa (1334 KK) hadi alipofariki dunia (1323 KK). Alikuwa farao wa nasaba ya 18 (familia ya kifalme) wakati wa Ufalme Mpya.
Yeye ni mashuhuri kwa sababu kaburi lake ni kaburi pekee kati ya makaburi yote ya kifalme ya Misri ya Kale lililohifadhiwa bila kuporwa mali hadi karne ya 20.