Tuzo ya Nobel ni tuzo ya fedha kwa ajili ya mafanikio ya pekee katika fani mbalimbali. Ilianzishwa na Alfred Nobel.
Tangu mwaka wa 1901 imetolewa kwa watu waliofaulu katika fani zifuatazo: Fizikia, Kemia, Tiba (au Fiziolojia), Fasihi na Amani. Tangu mwaka wa 1969, tuzo ya sita imeongezwa kwa Uchumi. Siku hizi Tuzo ya Nobel ni tuzo ya kimataifa mashuhuri zaidi duniani. Wanaotuzwa hupokea hati, medali ya dhahabu na kiasi cha pesa cha takriban € milioni 1,2 (kinategemea mapato ya riba yanayotokana na mfuko wa fedha iliyotengwa na Alfred Nobel kwa kusudi hili).
Maazimio kuhusu tuzo za kila mwaka hutolewa kufuatana na wasia wa Alfred Nobel na kamati zifuatazo: