Tuzo ya Pulitzer ya Wasifu ni aina moja ya Tuzo za Pulitzer ambazo hutolewa kila mwaka nchini Marekani. Ni miongoni mwa aina za asili zilizotolewa kuanzia 1917, na imetolewa kumheshimu mwandishi Mwarekani aliyeandika wasifu wa mtu hodari katika mwaka uliopita.
Kuanzia 1980, wagombea watatu wa mwisho walikuwa hutangazwa, yaani mshindi mkuu pamoja na mshindi wa pili na wa tatu.