Uafrocentriki

Uafroncentriki (kutoka Kiingereza: Afrocentrism vilevile huitwa Afrocentricity) ni itikadi ya kitamaduni au mtazamo wa kilimwengu ambao hasa ulitolewa na wasomi Weusi wanaoishi nchini Marekani na imejikita katika kuelezea historia ya mtu mweusi Ni majibu yaliyotokana na toleo la ulimwengu la (Eurocentriki) kuhusu Watu wa Afrika na michango yao kihistoria na vilevile katika kutaka kujua asili yao na itikadi zao. Afrocentricity inajishughulisha hasa elimu ya kujitambua kusimama kama wakala wa Afrika na itakadi nzima ya Pan-African na utamaduni wake, falsafa, na historia.[1][2] Vilevile Afrocentric hutazamiwa kama mawazo ya Wasomi wa Kiafrika na kwingineko ambao walisoma huko Ulaya. Wengi wao waliibuka katika karne ya 20 hasa kipindi kile cha harakati za kupigania uhuru na ukoloni barani Afrika. Kwa mujibu wa wasomi hao, sababu zilizopelekea Unyang'anyi wa Afrika ni kwa sababu ya mapinduzi ya viwanda ambayo yalichukua nafasi barani Ulaya katika karne ya 19. Mapinduzi hayo yalikuwa na changamoto mbalimbali kwa mataifa ya Ulaya. Ili kuondoa changamoto hizo, wakaona bora waje Afrika - jambo ambalo lilipelekea kuigawa Afrika kwa mataifa yenye nguvu ya Ulaya.

  1. Asante on Afrocentricity Ilihifadhiwa 23 Novemba 2018 kwenye Wayback Machine..
  2. Africana: The Encyclopedia of the African and African-American Volume 1., p. 111 by Henry Louis Gates (Editor), Kwame Anthony Appiah (Editor) Oxford University Press. 2005.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne