Ubaldeska

Mt. Ubaldeska alivyochorwa.

Ubaldeska (jina kamili la Kiitalia: Ubaldesca Taccini; Calcinaia, Italia, 1136 - Pisa, Italia, 1206) alikuwa bikira aliyemfuata tangu ujanani[1] Yesu Kristo katika familia ya kiroho ya Utawa wa Mt. Yohane.

Kwa miaka 55 alitekeleza matendo ya huruma katika hospitali ya utawa huo[2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Mei[3].

  1. Salani, Massimo. " Santa Ubaldesca Taccini Vergine dell'Ordine di Malta", Santi e Beati, December 3, 2001
  2. "St. Ubaldesca - Virgin of the Order of Malta". www.smom-za.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-02. Iliwekwa mnamo 2017-05-19. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  3. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne