Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 2007

Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi


Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya ulikuwa na matatizo mengi na kusababisha machafuko yaliyopelekea kutokea kwa vifo. Katika kadhia hii, watu 1,300 walipoteza maisha na wengine 300,000 kujeruhiwa.[1]

Baada ya Raila Odinga wa ODM kuongoza katika hesabu ya kura kwa muda mrefu Tume ya Uchaguzi ya Kenya lilisimamisha hesabu kwa muda wa usiku mmoja na baada ya kuanza upya kura za Mwai Kibaki wa PNU zilikuwa mbele. Tume ikamtangaza Kibaki kuwa mshindi naye aliapishwa mara moja bila kusubiri muda wa kisheria kwa malalamiko. Watazamaji waliona kasoro, makosa na matokeo yaliyodokeza ya kwamba hesabu ya kura ilibadilishwa kwenye ngazi za kupiga jumla za kura kimkoa na kitaifa. Vilevile kuna madokezo ya kwamba kura za kirais ziliongezwa katika usiku ambako hesabu ilisimamishwa.

Matokeo yaliyotangazwa ni kama yafuatayo:

Wagombea wengine walimaliza kwa kura chache tu.

  1. "ICC inaashiria kupata nafasi ya kuwakabili watuhumiwa wa vurugu za uchaguzi nchini Kenya – DW – 31.07.2009". dw.com. Iliwekwa mnamo 2024-11-01.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne