| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Pravda vítězí (Kicheki: "Ukweli hushinda") | |||||
Wimbo wa taifa: Kde domov můj | |||||
Mji mkuu | Praha | ||||
Mji mkubwa nchini | Praha | ||||
Lugha rasmi | Kicheki | ||||
Serikali | Jamhuri Petr Pavel Petr Fiala | ||||
' Kutokea kwa taifa Uhuru kutoka Austria-Hungaria Mwisho wa Chekoslovakia |
Karne ya 9 (Dola la Moravia) 28 Oktoba 1918 1 Januari 1993 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
78,866 km² (ya 117) 2.0 | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2021 sensa - Msongamano wa watu |
10,827,529 (ya 85) 10,524,167 133/km² (ya 91) | ||||
Fedha | Koruna (CZK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .cz 3 | ||||
Kodi ya simu | +4201
|
Ucheki au Chekia au Czechia (kwa Kicheki: Česko) pia Jamhuri ya Kicheki au Jamhuri ya Czech (kwa Kicheki: Česká republika) ni nchi ya Ulaya ya Kati na mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Imepakana na Poland, Ujerumani, Austria na Slovakia.
Mji mkuu ni Praha (Kijer.: Prag; Kiing.: Prague).
Miji mingine mikubwa ni Brno, Ostrava, Zlín, Plzeň, Pardubice, Hradec Králové, České Budějovice, Liberec, Olomouc na Ústí nad Labem.
Tangu zamani nchi imekuwa na kanda za Bohemia, Moravia na Silesia.
Wakazi husema hasa Kicheki ambacho ni lugha ya Kislavoni ya Magharibi.
Ni kati ya nchi ambako dini si muhimu kimaisha. Wakati wa sensa ya mwaka 2021, 56.9% ya wakazi walisema hawana dini yoyote, 30.1% hawakujibu swali husika, 11.7% walijitambulisha kama Wakristo (Wakatoliki 9.3% na madhehebu mengine 2.4%).