Udeni

Kongeriget Danmark (Kideni)
Ufalme wa Udeni
Bendera ya Denmark Nembo ya Denmark
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: hakuna
Wimbo wa taifa: Der er et yndigt land (kitaifa);
Kong Christian (kifalme)
Lokeshen ya Denmark
Mji mkuu Kopenhagen
55°43′ N 12°34′ E
Mji mkubwa nchini Kopenhagen
Lugha rasmi Kideni1
Serikali Ufalme wa kikatiba
Frederik X
Mette Frederiksen
Kuungana kwa nchi
{{{established_events}}}
mnamo 980 BK
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
43,094 km² (ya 1341)
1.6%1
Idadi ya watu
 - 2024 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
5,982,117 (ya 112)
138.8/km² (ya 933)
Fedha Kroner (DKK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET3 (UTC+1)
CEST3 (UTC+2)
Intaneti TLD {{{cctld}}}
Kodi ya simu +453
1 Habari zote za Udeni bila Faroe na Grinilandi.


Ramani ya Udeni

Udeni (en: Denmark, da: Danmark ) ni nchi iliyoko kaskazini mwa Ulaya, na ni sehemu ya ufalme wa Denmark, ambayo pia inajumuisha Greenland na Visiwa vya Faroe. Nchi hii ina mipaka na Ujerumani upande wa kusini, huku upande wa kaskazini ikiwa na bahari ya Kaskazini na upande wa mashariki ikiwa na bahari ya Baltiki.

Mji mkuu wa Denmark ni Copenhagen, ambao ni jiji kuu na kitovu cha uchumi, biashara, na utamaduni nchini.

Imepakana na Ujerumani upande wa kusini na kuzungukwa na maji pande tatu zilizobaki. Kaskazini kwake iko Norwei ng'ambo ya mlango wa bahari ya Skagerak, mashariki iko Uswidi ng'ambo ya Kattegat na Oresund. Bahari ya Kaskazini iko upande wa magharibi, Baltiki inaanza kwenye visiwa vikuu vya Udeni.

Greenland na visiwa vya Faroe ni sehemu ya ufalme wa Udeni lakini zinajitawala.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne