Ufini

Jamhuri ya Ufini
Suomen tasavalta (Kifini)
Republiken Finland
(Kiswidi)
Wimbo wa taifa: "Maamme" (Kifini)
"Vårt land" (Kiswidi)
("Nchi yetu" Kiswahili)
Eneo la Ufini kati Umoja wa Ulaya
Ufini katika dunia
Mji mkuu
na mkubwa
Helsinki
Lugha rasmiKifini (89.33%), Kiswidi (5.34%)
SerikaliBunge la Jamhuri
 • Rais
Alexander Stubb
 • Waziri Mkuu
Petteri Orpo
 • Uhuru
6 Desemba 1917
 • Utambuzi wa uhuru
3 Januari 1918
Eneo
 • Jumlakm2 338,145 (ya ya 64)
 • Maji (asilimia)9.4%
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2024increase 5,635,560 [1]
 • Msongamano16/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2024
 • Jumlaincrease $351.5 bilioni [2] (ya 50)
 • Kwa kila mtuincrease $64,660 [3] (ya 23)
PLT (kawaida)Kadirio la 2024
 • Jumlaincrease $306.08 bilioni (ya 49) [3]
 • Kwa kila mtuincrease $54,770 [3] (ya 15)
HDI (2022)increase 0.942
SarafuEuro (€)
Majira ya saaUTC+2 EET
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+358
Jina la kikoa.fi
Pielinen

Ufini (kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu. Mji mkuu ni Helsinki; mji muhimu mwingine ni Tampere, mji ulioko karibu kilomita 180 kaskazini mwa Helsinki, ni wa pili kwa ukubwa. Miji mingine mikubwa ni pamoja na Turku, Kuopio na Vaasa.

Ufini ilijitegemea mnamo 1917. Kati ya 1939 na 1944, Ufini ilipigana dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na jeshi la Ufini liliongozwa na kamanda Carl Gustaf Emil Mannerheim.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.

  1. "Finland population 2024". 2024.
  2. IMF. "Plt ya Ufini" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-20.
  3. 3.0 3.1 3.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named auto1

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne