| |||||
Lugha rasmi | Kiswahili Kiingereza | ||||
Mji Mkuu | Kampala | ||||
Mji Mkubwa | Kampala | ||||
Serikali | Jamhuri | ||||
Rais | Yoweri Museveni | ||||
Eneo | km² 241,038 | ||||
Idadi ya wakazi | 42,729,036 (2018) | ||||
Wakazi kwa km² | 177 | ||||
Jumla la pato la taifa kinaganaga | Bilioni $46.38[1] | ||||
Jumla la pato la taifa kwa kila mtu | $1,060.43[1] | ||||
Pesa | Shilingi ya Uganda | ||||
Kaulimbiu | "kwa mungu na nchi yangu" | ||||
Wimbo wa Taifa | Ewe Uganda, Ardhi ya Uzuri/Urembo | ||||
Saa za Eneo | UTC +3 (Wakati wa Afrika Mashariki) | ||||
Mtandao | .ug | ||||
Kodi ya Simu | +256 |
Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini.
Uganda inamiliki sehemu ya ziwa la Viktoria Nyanza ikipakana huko na Kenya na Tanzania.
Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.