Uislamu nchini Mozambique

Uislamu kwa nchi

Uislamu nchini Mozambique ni dini inayokadiriwa kuwa na wafuasi wakifikiao asilimia 17.9 ya wakazi wote wa nchini humo.[1]

Sehemu kubwa ya Waislamu wa Mozambique ni wale wa dhehebu la Sunni wanaofuata mafundisho ya imamu Shafi, japokuwa kuna Waislamu wachache wa dhehebu la Shia ambao pia wamejisajili.

Waislamu nchini wanajumuishwa na Wamozambique wenyewe, raia wenye asili ya Asia Kusini (Wahindi na Wapakistani), na idadi ndogo kabisa ya wahamiaji wa Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Msikiti katika Kisiwa cha Mozambique
  1. "Uislamu nchini Msumbiji kwa Kireno". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2016-05-13.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne