Uislamu kwa nchi |
Uislamu nchini Armenia ulianza milimani au katika nyanda za juu hasa katika kipindi cha karne ya 7.
Waarabu, na baadaye kabila la Wakurdi, walianza kuloea Armenia hasa kwa kufuatia uvamizi wa Waarabu na kucheza nafasi kubwa kiitikadi, kijamii, kiuchumi na kihistoria nchini.[1]
Baada ya uvamizi wa Waseljuki katika karne ya 12, elementi za Waturuki hatimaye zikashinda uwepo wa Waarabu na Wakurdi. Kwa kuanzishwa kwa nasaba za Kiajemi kama vile Nasaba ya Safavid, Nasaba ya Afsharid, Nasaba ya Zand na Nasaba ya Qajar, Armenia ikawa kiungo muhimu cha ulimwengu wa Shia ya Kiajemi, huku ikiwa bado inaheshimu uhusiano na uwepo wa Ukristo nchini humo.