Ujenzi

Ujenzi wa ghorofa nyingi unahitaji teknolojia ya kisasa
Ujenzi wa kisiwa chenye umbo la mtende huko Jumeira, Dubai
Wajenzi kazini
Ujenzi wa daraja huko Ottawa, Kanada

Ujenzi ni teknolojia ya kujenga nyumba, viwanda, barabara, daraja au hata miji. Ujenzi ni kazi inayohusisha watu wengi na ngazi mbalimbali ya kupanga na kutekeleza.

Majengo madogo yajengwa na watu wenyewe kufuatana na maarifa yao bila mpangilio mkubwa. Wajenzi hutumia maarifa ya watu waliowatangulia.

Majengo makubwa zaidi huhitaji mpangilio mwangalifu. Mwenye jengo atatafuta kwanza ushauri wa wataalamu.

Msanifu atachora ramani. Wataalamu wengine hukadiria mahitaji ya vifaa na gharama za jengo. Vibali vinahitajika.

Wajenzi watakaa na kupanga mahitaji ya muda, pesa, wafanyakazi na mashine. Wahandisi na mafundi wa fani mbalimbali hushirikiana.

Utekelezaji unasimamiwa na msanifu pamoja na wataalamu wengine. Ni muhimu kuhakikisha ubora wa vifaa vinavyotumika wakati wa kujenga kwa kila hatua. Vipimo vinapaswa kufuatwa kwa umakini. Kama msingi una makosa jengo lote linaweza kukaa bila kumalizika wakati gharama kubwa zimeshapotea.

Jengo zuri litakaa muda mrefu. Lakini hakuna majengo ya kisasa yatakayodumu kama piramidi za Misri!


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne